Germain Katanga,kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la FRPI nchini DRC |
Jaji kiongozi katika kesi hiyo,Bruno Cotte amesema kuwa mahakama imemkuta na hataia ya kushiriki kupanga njama na kutekeleza mauaji dhidi ya raia kwenye mji wa Bogoro. Hata hivyo Jaji Cotte amesema kuwa miaka saba ambayo Katanga ametumia akiwa kizuizini itaondolewa kwenye hukumu hiyo iliyotollewa jana Ijumaa.
Katanga mwenye umri wa miaka 36, alikamatwa mwezi Machi kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwemo mauaji na unyang'anyi, na kwa kushiriki katika mashambulizi ya kijiji cha Bogoro Mashariki mwa DRC mnamo Februari 24, 2003.
Majaji wamegundua kuwa aliwapa silaha wapiganaji wa kundi la Patriotic Resistance Forces (FRPI) mjini Ituri ambao walifanya mauaji ya halaiki kijijini hapo na kuua watu zaidi ya 200.
No comments:
Post a Comment