Tuesday 13 May 2014

waziri Mkuu wa China akutana na Spika wa Bunge la Nigeria

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo asubuhi , Beijing amekutana na spika wa baraza la juu la bunge la Nigeria Bw. David Mark.
Bw. Li amezungumzia ziara aliyomaliza hivi karibuni nchini Nigeria na nchi nyingine za Afrika akisema, kupitia ziara yake, ameiona Nigeria inayoibuka na bara la Afrika lenye matumaini. Amesema China inapenda kushirikiana na Nigeria na nchi nyingine za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, hasa kuongeza biashara na uwekezaji, kutekeleza kwa ubora miradi mikubwa ya ushirikiano, na kuongeza mawasialiano ya kiutamaduni.
Kwa upande wake, Mark amesema Bw. Li alifanya ziara nchini Nigeria wakati nchi hiyo ikikabiliwa na matatizo, ziara hiyo sio tu inaonesha urafiki wa dhati kati ya China na Nigeria, bali pia ni uungaji mkono wa kithabiti kwa Nigeria, na kuitia moyo serikali na watu wa Nigeria. Nigeria inakaribisha kampuni za China kuwekeza nchini humo, na itatoa urahisi kwa kampuni hizoa na kuhakikisha usalama wa watu wake na mali zake.

No comments: