Saturday, 17 May 2014

Mtanzania Adam Ndita na wenzake waifundisha man U mpira juzi

 Beki wa kushoto wa Chelsea, Mtanzania Adam Nditi (kulia) akiwania mpira na Tom Lawrence wa Manchester United juzi usiku kwenye Uwanja wa Old Trafford.
 MTANZANIA, Adam Nditi, ameiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa soka la vijana wenye umri chini ya miaka 21 huku akicheza dakika zote 90.
Nditi aliyezaliwa Zanzibar Septemba 18, 1994 alicheza nafasi ya beki wa kushoto katika kikosi hicho kilichotwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Manchester United mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford juzi Jumatano.
Hata hivyo, Nditi alionyeshwa kadi ya njano katika mchezo huo sambamba na mwenzake, John Swift. Wote ni kutokana na mchezo usiofaa kwa wapinzani wao.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na kocha wa muda wa Man United, Ryan Giggs na msaidizi wake, Paul Scholes, mabao ya Chelsea yalifungwa na Charly Musonda na Lewis Baker katika dakika za 21 na 78.
Man United ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa Tom Lawrence ambalo lilishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wake waliokuwa nyumbani lakini baadaye mambo yaliwabadilikia.

No comments: