Sunday 18 May 2014

Usalama kuimarishwa Nigeria

Macho yote duniani yatazama Nigeria baada ya wanafunzi wa kike zaidi ya 200 kutekwa nyara nchini humo.
mkutano-wa-usalama-nigeria
Marekani na Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Uingereza walifanya ‘’Mkutano wa Usalama Nigeria’’ katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
Rais François Hollande ambaye ni mwenyeji, aliungana na rais wa Nigeria Goodluck Jonathan pamoja ni viongozi wa Benin, Cameroun, Niger na Chad kuhudhuria katika mkutano huo.
Kufuatia mkutano huo, mkutano wa waandishi wa habari uliohudhuriwa na viongozi wa Afrika pia ulifanyika.
Katika mkutano huo, rais wa Ufaransa alisema kwamba kwa mwelekeo wa kimataifa, wameamua kupambana na mashirika ya kigaidi.
Hollande aliashiria ya kuwa raslimali za fedha na silaha zinazomilikiwa na mashirika ya kigaidi zinahitaji kusitishwa.

No comments: