Waziri
wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi jana usiku alizungumza na naibu
waziri mkuu wa Vietnam ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje ya nchi hiyo
Bw. Pham Binh minh kwa njia ya simu, ambapo aliilaani vikali Vietnam
kutokana na vitendo vya kushambulia kampuni za China vinavyotokea nchini
Vietnam. Hivi karibuni mashambulizi dhidi ya wawekezaji kutoka nje
yalitokea nchini Vietnam, baadhi ya kampuni za China, Singapore na Korea
Kusini zilishambuliwa, na kusababisha kifo cha raia mmoja wa China,
wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, na hasara kubwa ya mali.
Bw.
Wang Yi amesema Vietnam inapaswa kuwajibika na mashambulizi dhidi ya
kampuni na watu wa China, na China inaitaka Vietnam ichukue hatua zenye
ufanisi, kuzuia vitendo vya kimabavu, kulinda usalama wa kampuni na watu
wote wa China, kuwatibu majeruhi, kuanza uchunguzi kuhusu mashambulizi
hayo, kuwaadhibu wahalifu wote, na kutoa fidia kwa kampuni na watu
walioathiriwa.
Naye Bw. Pham Binh Minh amesema, Vietnam imewakamata
watuhumiwa zaidi ya 1000, na itachukua hatua zote kulinda usalama wa
kampuni na watu wa China nchini humo.
No comments:
Post a Comment