Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari mjini |
Habari zilizolifikia gazeti hili zilisema jana
kuwa siyo tu Serikali imesogeza mbele Bajeti ya Wizara ya Maji, bali pia
hata ya Wizara ya Nishati na Madini na sasa zitasomwa mwezi ujao baada
ya kubaini kuwa wabunge wengi wamekamia kuzikwamisha kutokana na miradi
mingi iliyopangwa mwaka jana kutokamilika.
Wizara ya Maji ilikuwa iwasilishe bajeti yake leo
bungeni wakati bajeti ya Nishati na Madini ilikuwa imepangwa
kuwasilishwa Mei 23.
Katika kile kinachoonekana ni Serikali kusoma
alama za nyakati, imemwandikia Barua Spika wa Bunge, Anne Makinda
ikimwomba zisogezwe mbele.
Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi imependekeza bajeti
hizo zisogezwe mbele hadi Juni.
Lukuvi jana alithibitisha kumwandikia Spika barua
akiomba kusogezwa mbele kwa bajeti hizo akisema ni kutokana na
mazungumzo yanayoendelea kati ya Hazina na wizara hizo kuhusu fedha
zinazohitajika.
Hata hivyo, chanzo chetu kimeeleza kwamba lengo la
Serikali kusogeza mbele bajeti hizo ni ‘janja’ ya kusubiri munkari wa
wabunge utulie baada ya kupitisha bajeti za wizara nyingine zisizokuwa
na maswali mengi.
Akizungumzia suala hilo Lukuvi alisema: “Bajeti ya
Maji hatuiahirishi kwa sababu ya Mnyika, hapana! Nilishamwandikia barua
Spika siku nyingi… Hii ya Maji haitasomwa kesho (leo) kwa sababu bado
hawajaweka bajeti zao vizuri,” alisema.
Lukuvi alisema baada ya Spika kupokea barua hiyo,
alimweleza kuwa ni lazima Kamati ya Uongozi ya Bunge ikutane na
itakutana leo na kuna uwezekano leo ikasomwa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa badala ya Maji.
Wakati Lukuvi akisema kuna mazungumzo na Hazina, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alipoulizwa jana alisema hajui chochote.
Madai ya Mnyika
Akizungumza na waandishi wa habari bungeni jana,
Mnyika alisema lengo lake ni kutaka bajeti hiyo irejeshwe kwenye Kamati
ya Bajeti kwa ajili ya kupitiwa upya.
No comments:
Post a Comment