Wednesday 21 May 2014

Wanawake wanaokula Udongo wako hatarin kuzaa watoto wasio na akili timamu

Udongo unaoliwa na wanawake katika baadhi ya nchi Afrika
Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.
Utafiti uliofanywa na shirika la African Council for Gifted and Talented unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawamakiniki darasani.
Mkuu wa shirika hilo Profesa Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa utafiti huo umefanywa kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo hujihusisha kutambua na kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.
Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.
Mtoto akiwa kwenye tumbo la mamake
Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa huchelewa kushika mambo.
Wasimamizi wa mradi huo waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.
Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.

No comments: