Monday, 26 May 2014

20 wafa kwa ajali ya tren IndiaMaafisa wa huduma za treni nchini India wanasema kuwa takriban watu 20 wanahofiwa kufariki katika ajali ya gari moshi katika jimbo la Uttar Pradesh.
Treni hiyo ya kubeba abiria iligongana na treni ya jizigo iliyokuwa imeemgeshwa katika kituo cha treni cha Chureb.
Mabehewa sita ya treni hiyo ya Gorakhdham Express yaling'oka kutoka kwenye treni hiyo.
Waokozi wanajaribu kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo na ambao bado wamekwama.
Treni hiyo ilikuwa inasafiri kutoka mjini Gorakhpur hadi katika jimbo la Hisar Haryana

No comments: