Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inayozidi
kuzorota kila uchao imesababisha uchumi nao kuendelea kuporomoka ambapo
Umoja wa Mataifa umesema unaweka vipaumbele vya usaidizi kwa kuzingatia
rasimu ya mpango ulioandaliwa na serikali ili kukwamua nchi hiyo. Ripoti
kamili na Alice Kariuki.
(Taarifa ya Alice)
Uimarishaji wa ulinzi na usalama, utawala bora, usaidizi wa
kibinadamu na maendeleo ya kiuchumi, hayo ni mambo manne ambayo Ofisi ya
Umoja huo inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA imetaja
kuzingatia katika operesheni zake.
OCHA imesema watu Milioni Mbili na Nusu nchini humo ambao ni zaidi ya
nusu ya wakazi wa nchi hiyo sasa wanahitaji usaidizi kwani shughuli za
kujipatia kipato zimekwama, usalama unazidi kuporomoka. Hata hivyo
Claire Bourgeois mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini humo anasema
wanachofanya sasa ni..
(Sauti ya Claire)
"Kutoa huduma za kuokoa maisha kwa wakimbizi wa ndani na
jamii, na pili kuhakikisha walioathiriwa na mzozo wanalindwa hususan
makundi yaliyo hatarini. Ndio maana tunazingatia mambo hayo mawili na
kujikita katika kujenga uwezo kwa jamii zilizoathirika ziweze
kustahimili na ndio maana tunataka wadau wa maendeleo wajumuike kwani
hatimaye tunataka jamii irejee nyumbani na kuendelea na maisha yao
Jamhuri ya Afrika ya Kati."
Ombi jipya la fedha kwa usaidizi ni dola Milioni 551 na kiasi kilichopatikana hadi sasa ni asilimia 30 pekee.
No comments:
Post a Comment