Saturday, 17 May 2014

Sudan yatoa wito kwa pande mbili zinazopambana za Sudan Kusini kufuata makubaliano ya kusimamisha vita

Sudan imetoa wito kwa pande mbili zinazopambana nchini Sudan Kusini kuheshimu makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa tarehe 9, Mei, na kufungua njia ili misaada ya kibinadamu iwafikie wananchi wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Sudan imeeleza wasiwasi mkubwa wa nchi hiyo kuhusu mapambano yaliyotokea katika majimbo ya Jonglei, Upper Nile na Unity. Imesisitiza kuwa mgogoro wa Sudan Kusini unaathiri amani na usalama wa nchi za kanda hiyo, hasa Sudan.
Wakati huohuo, Kamati ya Kimataifa ya Chama cha Msalaba Mwekundu (ICRC) imesema inahitaji Dola za Kimarekani milioni 55 ili kutoa msaada wa kibinadamu kwa Sudan Kusini.

No comments: