Saturday 17 May 2014

Boko Haramu waendelea Kuishambulia Nigeria

Boko Haram waendelea kushambulia nchini NigeriaKundi la Boko Haram limeripotiwa kuendelea kufanya mashambulizi nchini Nigeria, ambapo msemaji wa jeshi la nchi hiyo ametangaza kuwa, wanamgambo wa kundi hilo wamechoma moto shule mbili. Imeelezwa kuwa, makumi ya wanamgambo wa kundi hilo wameshambulia vijiji viwili kaskazini mwa Nigeria na kuchoma moto shule mbili lakini hakuna mtu aliyeuawa au kujeruhiwa.
Hayo yanajiri huku jeshi la Nigeria likisaidiwa na wanajeshi kutoka nchi kadhaa likiendelea kuwasaka wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo. Wakati huo huo wabunge wa Nigeria wanajadili juu ya kuongeza muda wa sheria ya hali ya hatari iliyotangazwa kaskazini mashariki mwa Nigeria. Rais Goodluk Jonathan ametaka muda wa sheria hiyo uongezwe ili kukabiliana na mashambulio ya Boko Haram

No comments: