Tuesday, 28 February 2017

Mbowe atinga mahakamani kusikiliza kesi ya Lema


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akiwa ameongozana na Mbunge wa Kibamba wakiwasili katika Mahakama Kuu Mkoa wa Arusha Leo Jumatatu 27/02/2017 ikiwa leo linasikilizwa shauri la Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Godbless Lema.
Viongozi wengine waliofika mahakamani leo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, Mjumbe wa Kamati Kuu,Prof. Mwesiga Baregu, Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye, Meya wa jiji la Arusha,Mhe. Calist Lazaro, Katibu wa CHADEMA Arusha, Mhe. Aman Golugwa na viongozi mbalimbali wa CHADEMA

Thursday, 16 February 2017

baraza la mitihani Tanzania la hairisha zoezi la udahili

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule za sekondari za serikali uliokuwa ufanyike Februari 28, mwaka huu. Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Salumu alisema hayo juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa
akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.
Salumu alisema mpango wa kuwafanyia mtihani wa udahili wanafunzi hao ulitokana na matakwa yaliyowasilishwa Necta na baadhi ya wakuu wa shule za serikali wakipendekeza kupitia maofisa
elimu wa mikoa na wilaya kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliochaguliwa na kupangiwa shule zao wengi hawana sifa na uwezo wa kumudu masomo. Naibu Katibu Mtendaji wa Necta alisema wakuu wa shule walikuwa wakiomba kupata idhini ya kuwafanyia mtihani wanafunzi ili kubaini uwezo wao na kwamba baraza liliwasiliana na maofisa elimu mkoa na wilaya likiwataka kuwasilisha orodha ya idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa kwenye shule ya zao.
Alisema baada ya kufahamika idadi ya wanafunzi hao, baraza ndilo litatunga maswali ya mitihani yenye kuzingatia mfumo na vigezo maalumu na kutumiwa wakuu wa shule hizo ili kuusimamia kwa lengo la kuweka uzani sawa wa mtihani huo.

Kichanga atupwa, wapita njia wamuokoa

Mtoto aliyetupwa na kuokotwa akiwa katika Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Ifisi, Mbalizi Mbeya.

Sauti ya kilio cha kichanga wa kiume aliyekuwa ametupwa na mamaye asiyefahamika, kimeliondoa giza na kuwashitua wapita njia ambao wamemuokota akiwa hai.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema jana majira ya usiku wa saa tatu usiku kukiwa na baridi, walisikia sauti ya kulia kichanga mita 100 kutoka katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Kango kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wamesema waliposogea walimkuta mtoto huyo wa kiume akiwa ameviringishwa (visepe), katikati ya nyasi Jirani na Nyumba ambayo haikaliwi na mtu.
Baadae walimpeleka kituo cha Polisi Mbalizi ambako walipata msaada wa gari binafsi baada ya askari waliokuwepo kituoni kuwaambia kuwa gari la serikali halikuwa na mafuta.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mwanakikundi cha Taarifa na Maarifa kata ya Nsalala, Tausi Sanga alisema baada ya kumkuta mtoto huyo alihusika kumpeleka hospitali teule ya wilaya hiyo Ifisi.

Friday, 10 February 2017

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) jela miaka mitano kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni 5, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe kwa mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo, Mgawe ameachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo.
Mashitaka aliyokuwa anashitakiwa nayo ni ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam gati namba 13 na 14 kwa Sh trilioni moja mkataba walioingia na kampuni ya ujenzi ya China Communication Construction Company Limited (CCCCL).
Aidha, mahakama hiyo ilimwachia huru  aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Hamadi Koshuma baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.

Freeman Aikael Mbowe amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Paul Makonda

Breaking News........

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10 February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.
Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).
Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudhalilisha, na kukamata.
Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.
Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.

Wednesday, 8 February 2017

MCHUNGAJI LUSEKELO (MZEE WA UPAKO) ALAANI UTARATIBU UNAOTUMIKA KUWATAJA WATU BILA KUWA NA UHAKIKA WA KUTOSHA.

Mzee wa upako dakika chache zilizopita alipokuwa kwenye kipindi cha 'Kikaangoni' kinachorushwa moja kwa moja na EATV, amesema kuwa kilichopaswa kufanywa ni kuwaandikia summons washukiwa hao, kuwataka kuripoti polisi kwa mahojiano, na sio kuwaita kupitia magazeti, na kuwataja majina kwenye vyombo vya habari.
Mzee wa upako alipoulizwa swali kuhusiana na mchungaji Gwajima kutajwa na Makonda, amesema kuwa kumtaja mtu juu ya tuhuma hizi ni lazima kuwe na uhakika wa kutosha, kuwe na ushahidi wa kutosha, na sio kumtaja mtu bila ushahidi wa kutosha, ni kumdhalilisha mtu, kumshushia heshima yake, na kumsononesha moyoni.

Tuesday, 7 February 2017

Jeshi la polisi njombe lakamata vipondozi haramu zaidi ya tani 10

Mkuu wa mkoa wa njombe Mh Christopher Ole Sendeka  akishirikiana na vikosi vya Jeshi la Polisi Mkoani Njombe wamefanikiwa kukamata magari mawili ya kubeba Mafuta yakiwa yamebeba Vipodozi hatari kwa matumizi ya binadamuVyenye vinauzito wa Tan 10.      
        
 Kutokana na Tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amemwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Njombe,kushirikiana na TRA,TAKUKURU , TFDA na Wakala wa Barabara (TANROAD) kufutilia vipondozi hivyo vimeingiaje Nchini mpaka na vimepitaje toka Tunduma,Songwe,Mbeya mpaka kuja kukamatwa Mzani wa Makambako..   
Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi.