Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha
miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni 5, aliyekuwa Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe kwa mashitaka ya
matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo, Mgawe ameachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo.
Mashitaka aliyokuwa anashitakiwa nayo ni ya upanuzi wa
Bandari ya Dar es Salaam gati namba 13 na 14 kwa Sh trilioni moja
mkataba walioingia na kampuni ya ujenzi ya China Communication
Construction Company Limited (CCCCL).
Aidha, mahakama hiyo ilimwachia huru aliyekuwa Kaimu
Mkurugenzi wa TPA, Hamadi Koshuma baada ya upande wa mashitaka kushindwa
kuthibitisha mashitaka dhidi yake.
No comments:
Post a Comment