Sauti ya kilio cha kichanga wa kiume aliyekuwa ametupwa na
mamaye asiyefahamika, kimeliondoa giza na kuwashitua wapita njia ambao
wamemuokota akiwa hai.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema jana majira ya usiku wa
saa tatu usiku kukiwa na baridi, walisikia sauti ya kulia kichanga mita
100 kutoka katika kilabu cha pombe za kienyeji cha Kango kata ya Nsalala
Mbalizi Mbeya Vijijini.
Wamesema waliposogea walimkuta mtoto huyo wa kiume akiwa
ameviringishwa (visepe), katikati ya nyasi Jirani na Nyumba ambayo
haikaliwi na mtu.
Baadae walimpeleka kituo cha Polisi Mbalizi ambako walipata
msaada wa gari binafsi baada ya askari waliokuwepo kituoni kuwaambia
kuwa gari la serikali halikuwa na mafuta.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mwanakikundi
cha Taarifa na Maarifa kata ya Nsalala, Tausi Sanga alisema baada ya
kumkuta mtoto huyo alihusika kumpeleka hospitali teule ya wilaya hiyo
Ifisi.
"Tulipomfikisha Polisi na kuambiwa hawana mafuta kwenye
gari hatukupendezwa lakini kuna askari ni Trafiki akampigia mwenzake
simu akaja kutuchukua na gari yake binafsi na kutuleta hospitalini"
alisema Tausi alipokuwa na wanakikundi wenzake katika hospitali ya
Ifisi.
Muuguzi mkuu wa Hospitali hiyo Elmath Sanga alisema mtoto
huyo anaendelea vizuri na kuna muuguzi anamuhudumia kwa karibu ikiwemo
kumpatia maziwa.
"Hitaji kubwa la sasa ni nguo" alisema Muuguzi huyo mbele
ya Mwandishi wa habari na wanaharakati hao wa kikundi cha Taarifa na
Maarifa.
Baadhi ya wanakikundi cha Taarifa na maarifa kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya, wakiwa nje ya Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya baada ya kutoka kumuona mtoto waliyeshiriki kumuokota jana usiku na kumfikisha kituo cha Polisi Mbalizi kisha hospotalini hapo.
Baadhi ya wanakikundi cha Taarifa na maarifa kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya, wakiwa nje ya Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya baada ya kutoka kumuona mtoto waliyeshiriki kumuokota jana usiku na kumfikisha kituo cha Polisi Mbalizi kisha hospotalini hapo.
No comments:
Post a Comment