Mzee wa upako dakika chache zilizopita alipokuwa kwenye
kipindi cha 'Kikaangoni' kinachorushwa moja kwa moja na EATV, amesema
kuwa kilichopaswa kufanywa ni kuwaandikia summons washukiwa hao,
kuwataka kuripoti polisi kwa mahojiano, na sio kuwaita kupitia magazeti,
na kuwataja majina kwenye vyombo vya habari.
Mzee wa upako alipoulizwa swali kuhusiana na mchungaji
Gwajima kutajwa na Makonda, amesema kuwa kumtaja mtu juu ya tuhuma hizi
ni lazima kuwe na uhakika wa kutosha, kuwe na ushahidi wa kutosha, na
sio kumtaja mtu bila ushahidi wa kutosha, ni kumdhalilisha mtu,
kumshushia heshima yake, na kumsononesha moyoni.
Ametolea mfano kwake, kuwa mwaka 1997 aliwahi kutajwa kuwa
anauza madawa ya kulevya, lakini utaratibu uliotumika ni kwamba,
walimfuata Askari wa Interpol (mambo ya ndani), wakamuandikia summon ya
karatasi kuwa anahitajika polisi kwa mahojiano, alikwenda polisi
wakazungumza naye, akawaambia "ninyi ni polisi, fanyeni uchunguzi, "
basi polisi walipojiridhisha kuwa hahusiki, walimwacha huru, japo habari
ile ilivuja kwa vyombo vya habari na ikamchafulia jina kwa muda wa
takribani miaka Saba mpaka alipofanikiwa kuirejesha heshima yake.
Kwahiyo, Mzee wa upako amekazia kuwa, mtu kujijengea
heshima kwenye jamii inamchukua miaka mingi, kupata heshima sio kazi
ndogo, lakini inapokuja wakati unashushiwa heshima kwa sababu zisizo za
msingi, inaumiza sana.
No comments:
Post a Comment