Mbelgiji wa Simba atua MtibwaPiet de Mol akisaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo atasaidiwa na Meck Mexime aliyeifundisha timu hiyo kwa misimu mitatu
KOCHA Mbelgiji Piet de Mol amewasili Dar es Salaam leo na kupokewa na Mkurugenzi wa klabu ya mtibwa Sugar Jamal Bayser, ambaye watafanya mazungumzo kabla ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo na kumfanya kocha aliyeifundisha timu hiyo kwa misimu mitatu Mecky Maxime kuwa msaidizi wake
Piet de Mol alikuja Tanzania maalumu kwa ajili ya kuifundisha klabu ya Simba ambayo ilikuwa ikitafuta mrithi wa kocha wake aliyehitaji kiasi kikubwa cha fedha Goran Kopunovic, ambaye baadaye Mserbia huyo alikubali na kiasi cha pesa alichoahidiwa na uongozi wa Simba na kukubali kurudi kuifundisha Simba msimu ujao.
Kocha huyo mwenye miaka 60 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya anaweza kuibadilisha timu hiyo ambayo ilikuwa na msimu mbaya uliopita licha ya kuanza vizuri kwa kuongoza ligi ya Vodacom kwa kuongoza kwa muda mrefu.
Kopunovic alitaka dola za Kimarekani 50,000 sawa na Sh. Milioni 100 kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 Sh. Milioni 16.