Tuesday 19 May 2015

Ramsey atangazwa rasmi kuwa mkufunzi wa QPR

Chris Ramsey
Kilabu ya QPR imemuajiri Chris Ramsey kama mkufunzi mkuu kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Ramsey mwenye umri wa miaka 53 alipewa kazi hiyo hadi mwisho wa mwezi Februari baada ya Harry Redknapp kujiuzulu lakini alishindwa kuizuia kilabu hiyo kusalia katika ligi kuu ya Uingereza.
''Chris alipochukua ukufunzi wa timu hii tayari tulikuwa katika matatizo makubwa'', alisema mwenyekiti wa kilabu hiyo Tony Fernandes.
Licha ya kushushwa daraja,sisi kama bodi tumefurahishwa na kazi ya Ramsey aliyofanya.
QPR imeshinda mechi tatu kati ya 14 zilizosimamiwa na Ramsey huku wakitarajiwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Leicester

No comments: