Simba imezidi kukiimarisha kikosi chake cha msimu
ujao baada ya kufanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji wawili Nahodha
Hassan Isihaka na kiungo Said Ndemla
KAMATI ya Usajili ya klabu ya Simba, imezidi kukiimarisha kikosi
chake cha msimu ujao baada ya kufanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji
wawili Nahodha Hassan Isihaka na kiungo Said Ndemla.Kamati hiyo ililazimika kusafiri hadi Afrika Kusini kuwafuata wachezaji hao waliopo nchini humo na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki michuano ya COSAFA, na kuwasainisha mikataba hiyo ya miaka mitatu kila mmoja.
Baada ya kufanikisha zoezi hilo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya usajili Zacharia Hans Poppe, ameiambia ukomboz kuwa kocha wao Goran Kopunovic, ndiye aliyependekeza wachezaji hao kupewa miakataba mipya vaada ya kuvutiwa na kazi yao msimu uliopita.
“Unajua Kopunovic ndiye kocha tutakaye endelea naye msimu ujao na kabla hajaondoka kwenya mapumziko alituambie kuhakikisha wachezaji hawa tunawapa mikataba baada ya kuridhika na utendaji wao wa kazi na sisi tukaona nivyema tukatimiza maombi yake,”amesema Hans poppe.
Poppe amesema baada ya kumalizana na nyota hao kwa sasa wanageukia kwa wachezaji wengine ambao wangependa kuendelea nao msimu ujao akiwemo winga msumbufu Ramadhan Sinagano ‘Messi” ambaye hivi karibuni alikata dau la Tsh. Milioni 30, alizopewa na uongozi wa timu hiyo ili aongeze mkataba mpya huku yeye mwenyewe akitaha apewe Tsh Milioni 50 kama ilivyokuwa kwa kiungo Jonas Mkude aliyesaini mkataba mpya kwa Tsh. Milioni 60 desemba 2014.
No comments:
Post a Comment