Monday 11 May 2015

Wanamgambo 60 wa Boko Haram wauawa katika mapigano Cameroon


Wanamgambo 60 wa Boko Haram wauawa katika mapigano CameroonWanamgambo 60 wa Boko Haram wauawa katika mapigano Cameroon

Afisa wa kijeshi, ameripoti kuuawa kwa takribani wanamgambo 60 wa Boko Haramu, katika mapigano na wanajeshi wa Cameroon karibu na mpaka wa Nigeria.
Aboubakar Issa, Afisa wa jeshi la Cameroon amelifahamisha shirika la Anadolu kuwa takriban wanamgambo 100 walivuka mpaka kwa kutumia pikipiki Jumamosi usiku na kushambulia mji wa Zelevet uliopo kusini mwa Cameroon.
Aliongeza kusema kuwa wanamgambo hao walishambulia kambi  ya jeshi katika mji wa Kalashnikovs na kuwajeruhi wanajeshi 2.
Katika shambulio hilo wanamgambo 60 wa boko haram waliuawa.
Boko Haram, wameongeza mashambulizi nchini Cameroon katika miezi ya karibuni, na kusababisha mamlaka ya nchi ya Cameroon kuongeza vikosi vya ulinzi mpakani mwa Nigeria, kwa msaada wa vikosi vya Chad mwezi Januari.
Nchi ya Cameroon imejiunga pamoja na Nigeria, Niger na Chad katika kupambana dhidi ya Boko Haram.

No comments: