Tuesday, 26 May 2015

Majibu ya msemaji wa Ikulu yamweka njia panda Dk. Mengi

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema bado  anahofia usalama wa maisha yake kutokana na majibu  ya Msemaji wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Salva Rweyemamu, kuhusu  Zitto alimchongea Mengi kwa Rais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema majibu ya Msemaji wa Ikulu  Bw. Salva Rweyemamu kuwa Mhe. Rais hakuwahi kuwa na mawasiliano na Zitto Kabwe kama ilivyoelezwa, na kwamba hakufanya lolote kuhusu tuhuma zilizotolewa, kwa vile aliona ni jambo dogo na ni  upuuzi, yanamfanya aendelee kuhofia usalama wa maisha yake.
Hofu ya Dr Mengi inakuja baada ya kurejea kisa cha Mfalme wa Uingereza  cha  Mwaka 1170.
Post a Comment