Saturday 2 May 2015

Dawa ya kupima virusi vya Ebola iliyotengenezwa China yaidhinishwa na WHO


Dawa ya kupima virusi vya Ebola iliyotengenezwa China yaidhinishwa na WHO

(GMT+08:00) 2015-05-01 20:49:55
Shirika la afya duniani WHO hivi karibuni limetangaza kuidhinisha dawa ya kupima virusi vya Ebola iliyotengenezwa na kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Shanghai Zhijiang na kuiweka kwenye orodha yake ya manunuzi ya dawa.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya virusi vya Ebola ambaye pia ni mkuu wa tume ya dharura ya Ebola Bw. Peter Graaf jana alisema kwenye taarifa yake kuwa muda wa kupambana na Ebola ni wa dharura.
Amebainisha kuwa kabla ya nchi zote zilizokumbwa na ugonjwa huo kutokomeza virusi vya Ebola, virusi hivyo bado ni tishio duniani. Katika kipindi muhimu cha wiki kadhaa zijazo, kila mgonjwa wa virusi hivyo anatakiwa kushughulikiwa kwa makini.

No comments: