Katika nafasi hiyo Okwi amewashinda wachezaji Ramadhani Singano na Ibrahim Ajibu ambao walikuwa wakimfukuzia kwa kasi katika kuwania tuzo hiyo iliyotolewa kwa kuangalia mchango wa kila mmoja msimu huu.
Baada ya kutajwa mshindi wa tuzo hiyo Okwi ameiambia Ukomboz blog, anafurahi kuwa mchezaji bora ndani ya klabu yake anaamini itamuongezea hamasa ya kuendelea kujituma na kuipa mafanikia zaidi msimu ujao lakini pia ameshukuru wachezaji wenzake wote ambao walishirikiana nao na kuifikisha Simba hapo ilipo.
“Nashukuru kwa tuzo hiyo lakini kama timu bado tunakazi kubwa ya kuhakikisha Simba inafanya vizuri msimu ujao na kutwaa ubingwa wa Tanzania bara,”amesema Okwi.
Kipa mkongwe Ivo Mapunda ametwaa tuzo ya kipa bora kutokana na mchango wake ndani ya timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita wakati kiungo said Ndemla akichaguliwa kuwa kiungo bora chupukizi aliyeonyesha kiwango cha juu na kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mechi alizocheza.
No comments:
Post a Comment