Kada wa CCM Buni Ramole, amejipalia mkaa kutokana na kauli yake
kwamba helikopta ya Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo
ni mbovu na ingeweza kumuua.
Ndesamburo kupitia kampuni ya mawakili ya Materu,
amemtaka kada huyo kumlipa fidia ya Sh100 milioni na kumwomba radhi,
akieleza kuwa kauli hiyo imemdhalilisha na kumvurugia biashara.
Kada huyo wa CCM, anadaiwa kukodi helikopta hiyo
Aprili 18, mwaka huu na kwenda nayo katika mkutano wa hadhara wa chama
hicho tawala uliofanyika katika viwanja vya Pasua mjini Moshi.
Hata hivyo, baada ya ukomboz blog kuripoti tukio
hilo, kada huyo alijitokeza hadharani na kukanusha kwamba helikopta hiyo
hakuikodi kwa Ndesamburo bali kwa kampuni ya General Aviation Services
(T) Limited.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi za CCM
wilaya ya Moshi Mjini, kada huyo alienda mbali na kudai kuwa helikopta
hiyo aliyokuwa aitumie wakati wa kampeni Oktoba mwaka huu, ni mbovu na
ingeweza kumuua.
“Nimechukua (chopa) makusudi ili kuwaonyesha
wananchi kuwa Chopa si maendeleo. Watu wa Moshi wanafikiri Chopa ni
maendeleo, Chopa kazi yake ni kuvuta watu na nimeshaiagiza itakuja, hii
niliyokodisha awali ni mbovu kwanza ingeweza kuniua,” alisema kada huyo.
Hata hivyo, Ndesamburo kupitia mawakili wake hao,
amemwandikia barua kada huyo akimtaka akanushe madai hayo, kwani ni ya
kashfa na yanaathiri vibaya biashara yake ya Chopa.
”Kwa barua hii tunakutaka ndani ya siku saba,
utangaze kwenye vyombo vya habarii kwamba taarifa yako ilikuwa si ya
kweli na uombe radhi kwa mteja wetu na kumlipa fidia ya Sh100
Milioni,”imedai barua hiyo iliyoandikwa Mei 6 mwaka huu.
Mawakili hao wamedai kuwa wanayo maagizo ya
kumfikisha kada huyo mahakamani kama hatatimiza masharti hayo na
Ndesamburo atadai fidia kubwa zaidi ya Sh100 Milioni anazodai.
Akizungumza na ukomboz blog mwishoni mwa juma,
Ndesamburo alisema, kada huyo hakuwa ameikodi helIkopta hiyo kama
anavyodai, bali alipewa kama “ofa” ili akiridhika, ndiyo wafanye
biashara Oktoba.
“Tulimpa kama majaribio ili aone uzuri wa
helikopta na akiridhika, aje tufanye biashara Oktoba na aliridhika ndiyo
maana Aprili 21 akaja kuchukua bei zetu,”
lakini mpaka leo hakuilipia” alisisitiza Ndesamburo.
Ndesamburo alisisitiza kuwa helikopta yake ni nzima kwa viwango vyote vya kimataifa.
na ndio maana hata viongozi wengine wa CCM na taasisi nyingine huikodisha.
No comments:
Post a Comment