Saturday, 23 May 2015

Watu watano washikiliwa kwa shutma za kuhusika katika biashara ya viungo vya Albino

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limewakamata watu watano waliokuwa wamejificha katika hoteli moja iliyoko wilayani Kahama mkoani humo wakifanya biashara ya viungo vya binadamu vinavyodhaniwa kuwa nia vya alibino hali ambayo inaonyesha dhahiri kuwa imani potofu na vitendo vya kishirikina bado vinaendelea kufanyika.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amethibitisha kukamatwa watu hao akiwemo mwalimu wa shule ya msingi katunguru iliyoko katika tarafa ya msalala wilayani Kahama aliyetajwa kwa jina la bahati kirungu huku kamanda kamugisha akidai kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ili kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaojihusisha na biashara hiyo.
 
Aidha kamanda kamugisha amesema bado kunahitajika nguvu kubwa katika harakati za kukomesha biashara haramu ya viungo vya binadamu inayochafua sifa ta taifa huku akiwataka watanzania kushirikiana na jeshi la polisi kupambana na biashara hiyo ili kuwanusuru binadamu wenzetu wasio na hatia wanaofanyiwa vitendo vya kikatili

No comments: