Sunday, 31 May 2015

Wolfsburg yanyakuwa kombe la Ujerumani kwa mara ya kwanza

Wolfsburg yatwaa kombe la Ujerumani kwa mara ya kwanzaWolfsburg yanyakuwa kombe la Ujerumani na kumsindikiza Jurgen Klopp kwa huzuni.

Haikuwa shangwe na nderemo kwa Jurgen Klopp katika mechi yake ya mwisho kama meneja wa Dortmund alipolazwa kwa mabao 3 kwa 1 na Wolfsburg katika fainali ya kombe la Ujerumani.
Dortmund walitangulia kufunga kupitia mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang katika dakika ya 5 bali Wolfsburg hawakufa moyo na bidii yao ililipa katika dakika ya 22 pale kiungo Luiz Gustavo aliposawazisha.
Kevin de Bruyne na Bas Dost walifunga mabao ya pili na ya tatu ya Wolfsburg katika dakika ya 33 na 38 mtawalia.
Kipindi cha pili hakikuwa na mihemko kama kipindi cha kwanza na mechi ilisalia 3 - 1 mpaka kupulizwa kwa kipenga cha mwisho na Wolfsburg wakatawazwa mabingwa wa kombe la Ujerumani kwa mara ya kwanza.
Post a Comment