Hatimaye
miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid imemtimua kocha wa timu hiyo
Carlo Ancelotti baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa misimu miwili.
Kocha
huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania
kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani
Ulaya. Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu
haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa
kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha
gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya
kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa
Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu
na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. Rais wa Madrid
Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis
kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment