Monday 25 May 2015

Mwanamke mwenye miaka 65 ajifungua pacha wanne Ujerumani

Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 ajifungua pacha wanne UjerumaniRekodi mpya ya mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi aliyejifungua pacha wanne duniani

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 aliyekuwa na uja uzito, anaarifiwa kujifungua pacha wanne nchini Ujerumani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Suddeutsche Zeitung, mwanamke huyo kwa jina la Annegret R, alizaa pacha wanne siku ya Jumanne iliyopita katika hospitali ya Berlin. Watatu kati ya pacha hao ni wa jinsia ya kiume, na mmoja ni wa kike.
Watoto hao wenye uzani wa gramu za kati ya 655 na 960, walikuwa na urefu wa sentimita 30 hadi 35.
Watoto hao waliozaliwa katika wiki ya 26 ya uja uzito, wanaarifiwa kuwa na bahati ya kuweza kuishi ingawa bado hawajakua vizuri.
Annegret R aliyepata uja uzito kwa njia ya upandikizaji ambayo imepigwa marufuku nchini Ujerumani, anasemekana pia kuwa na watoto 13 na wajukuu 7.
Annegret R sasa ameweka rekodi mpya ya mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani aliyeweza kujifungua pacha wanne.

No comments: