Rais
wa Burundi, Pierre Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini Tanzania
saa moja baada ya kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi
mkuu wa majeshi yake Meja jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba
amempindua.
Jenerali huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri
ya kufungwa kwa kiwanja cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo
mipaka ya Burundi.Hata hivyo haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono generali Meja jenerali Godefroid Niyombare.naye msemaji wa rais wa Burundi ,amesema kwamba wanajeshi watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa viongozi nchini Tanzania,amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
No comments:
Post a Comment