Saturday, 30 May 2015

Tanesco imesema kutokea kwa hitilafu ya umeme kumesababisha mikoa ya Tanzania bara kukosa huduma

Shirika la umeme nchini Tanesco limesema kutokea kwa hitilafu ya umeme katika msongo wa kilovoti 30 kumeharibu kifaa cha kukata umeme na kusababisha  mikoa ya Tanzania bara kukosa huduma ya umeme kwa muda.
Akizungumza na waandishi wa habari meneja mahusiano wa Tanesco Bwana Adriani Severini amesema mikoa yote nchini ilikosa huduma ya umeme isipokuwa mikoa ya Mtwara, Kigoma na Lindi ambapo amesema kwa upande wa jiji la Dar es Salaam kuna baadhi ya maeneo yamekosa huduma ya umeme hususani inayotumia umeme wa msongo wa kv 11.
Post a Comment