
Matokeo ya Mechi mbili za ligi kuu ya England zilizochezwa hapo
jana,Manchester City iliwachabanga Swansea mabao 4-2 . Ni Wilfried Bony
ambaye mnamo dakika ya 90 lililopigilia msumali wa moto kwa Swansea
baada ya kufunga bao la nne.Lakini Yaya Toure yeye alizifumania nyavu
mara mbili dakika 21 na 74. , James Milner naye akifunga mnamo dakika ya
36. Huku katika mechi ya pili Arsenal wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya
Man united,ambapo kwa matokeo hayo sasa Arsenal wanaendelea kujiimarisha
katika nafasi ya tatu. Leo West Brom watakipiga na Chelsea katika dimba
la The Hawthons.
No comments:
Post a Comment