Serikali ya Somalia imemteua
waziri wa zamani wa ulinzi kuwa kamanda wa kikosi cha polisi cha nchi
hiyo kufuatia tishio la mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu.
Wadhifa huo ulikuwa wazi tangu Oktoba mwaka jana baada ya aliyekuwa mkuu wa polisi kufariki kutokana na ugonjwa wa moyo.
Uteuzi huo umekuja wakati hali ya usalama nchini humo hasa katika mji wa Mogadishu ikizorota kufuatia mashambulizi kadhaa yanayofanywa na wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kusababisha vifo vya watu karibu 100 wakiwemo maofisa wa serikali.

No comments:
Post a Comment