Monday 25 May 2015

Mazishi ya kiongozi wa upinzani alieuawa kwa kupigwa risasi jijini Bujumbura

Mazishi ya kiongozi wa upinzani alieuawa BurundiMazishi ya kiongozi wa upinzani alieuawa kwa kupigwa risasi jijini Bujumbura

Maelfu ya raia wa Burundi wamekusanyika katika shuhuli za mazishi ya mmoja wa viongozi wa upinzani alieuawa kwa kupigwa risasi jioni ya Jumamosi na watu wasiojulikana tarafani Ngagara.
Shuhuli za mazishi zilianzia katika mskiti unaopatika kata ya 10 tarafani Ngagara.
Zedi Feruzi alikuwa mwenyekiti wa chama cha UPD ambacho ni moja ya vyama pinzani nchini Burundi.
Viongozi wa asasi za kiraia na wale wa vyama pinzani walishiriki katika mazishi hayo.
Ripota wa shirika la habari la Anadolu alifahamisha kuwa hakuna muakilishi yeyote kutaka katika chama tawala wala serikali alieshiriki katika mazishi hayo.
Katika msafara wa mazishi hayo kulionekana mabango yaliokuwa yameandikwa maneno dhidi ya rais Pierre Nkurunziza.

No comments: