Maelezo zaidi yanaarifu kwamba simu hiyo iligundulika kuwa tumboni mwa mwanamke huyo baada ya kuanza kunguruma ndani.
Tukio hilo liliwacha wengi vinywa wazi na kufikishwa katika bunge la Jordan, na kuitaka serikali ijiuzulu.
Kwa mujibu wa taarifa za Gulf News, mwanamke anayetambulika kwa jina la Hanan Mahmoud Abdul Karim mwenye umri wa miaka 36, alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Amman.
Baada ya kujifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 4.8 na kurudi zake nyumbani, mwanamke huyo alianza kusikia mingurumo tumboni na kuhisi maumivu.
Papo hapo mwanamke huyo alifikishwa katika hospitali ya serikali ya Amman, na kugundulika kuwa na kitu chenye urefu wa sentimita 7 tumboni mwake baada ya kufanyiwa utafiti.
Baadaye akafanyiwa upasuaji na kutolewa simu kutoka kwenye tumbo lake.
Tukio hilo lilizua utata na kufikishwa bungeni na Salim Al Bataynah, na kuitaka serikali ilijiuzulu kutokana na kosa hilo kubwa lililofanyika.
Wizara ya Afya ya Jordan ilifahamisha kutokuwa na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo, na kutangaza kwamba itafanya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment