Viongozi wa madhehebu ya dini ya kikristo na kiislamu walianza tukio hilo kwa kuwakumbuka wapendwa wao kwa sala na dua.
Miongoni mwa watu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya ni
pamoja na mwanamitindo wa kimataifa Flaviana matata ambaye alishindwa
kujizuia kutokwa machozi wakati alipokuwa akisimulia tukio la kumpoteza
mama yake mzazi, huku mfanyakazi wa shirika la maendeleo la taifa ( NDC )
Stewart Alphonce pamoja na msanii wa muziki wa Hip hop nchini Joseph
Haule maarufu kama Profesa J, wakisema hali ya usafiri katika ziwa
victoria bado ingali tete.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao walihudhuria kumbukumbu
hiyo wameiomba serikali kuitangaza tarehe 21 mei kila mwaka kuwa ni siku
ya maombolezo ya kitaifa ili kuwakumbuka wahanga waliopoteza maisha yao
kwenye ajali ya meli ya Mv.Bukoba.
No comments:
Post a Comment