Watu
29 wameuawa kati mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua
ndani ya msikiti.
Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.Shambulizi hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri lililondeshwa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Wanagamabo hao walifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13.
Rais Buhari alisema kuwa kituo cha kijeshi kitawekwa katika mji wa Maiduguri kusadia kupigana na wanamgambo hao.
Rais Buhari akihutubia taifa punde baada ya kuapishwa alisema kuwa jeshi la taifa hilo litakita kambi yake katika mji huo wa Maiduguri ilikuitokomeza kabisa kundi hilo la waislamu la Boko Haram.
"Kwa ushirikiano na majirani zetu Cameroon, Chad, Niger na jumuia ya kimataifa na dhamira ambayo tutapata kutoka katika jeshi, Nafikiri itachukua muda mfupi zaidi kukabiliana nao."
Jenerali Buhari amesema tayari ameainisha msingi wa tatizo linalokabili nchi ya Nigeria, lakini amewataka raia wa nchi hiyo kuwa wavumilivu.
"Tumebaini matatizo makubwa matatu.
''Matatizo haya matatu makuu, Wanigeria wote wanafahamu na tunaomba ushirikiano wa wananchi wa Nigeria'',
''wasitarajie miujiza kutokea katika kuyapatia ufumbuzi matatizo haya katika kipindi cha miezi michache baada ya kutwaa madaraka kwa sababu uharibifu umechukua miaka mingi,
miaka kumi na sita ya utawala wa chama tawala cha nchi hii." Anasema rais huyo mpya wa Nigeria
No comments:
Post a Comment