Arsenal iliandikisha rekodi mpya ilipoicharaza Aston Villa kwa mabao 4 kwa bila katika mechi ya fainali ya kombe la FA. Arsenal iliipiku Manchester United kwa kuwa timu ya kwanza kushinda kombe hilo kwa mara ya 12. Arsenal sasa ndiyo timu yenye ufanisi mkubwa zaidi katika kombe la FA.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott katika dakika ya 40 , Alexis Sanchez kupitia mkwaju wa mbali katika dakika ya 50, Per Mertesacker kupitia mkwaju wa kichwa katika dakika ya 62 kabla ya mshambuliaji Olivier Giroud kumalizia katika dakika za lala salama.
Nahodha wa Arsenal Per Mertesacker alisema kuwa kufuatia ushindi wa pili wa FA timu hiyo inapaswa kuwa washindani wakali zaidi kwenye ligi kuu.

No comments:
Post a Comment