Monday, 1 June 2015

Mkutano wa viongoz wa EAU waadhimia uchaguzi wa Burundi kuhairishwa

Viongozi wa Afrika Mashariki wametoa wito kuwa uchaguzi wa Burundi uakhirishwe kwa angalau wiki sita na ghasia zimalizike.
Taarifa hiyo inafuatia mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Uamuzi wa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kuania muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi wa mwezi ujao, umesababisha maandamano kwa majuma kadha sasa.
Kiongozi wa Burundi hajakuwako kwenye mkutano huo.
Mara ya mwisho alipohudhuria mkutano kama huo awali mwezi May, maafisa wa jeshi walijaribu kumpindua.
Post a Comment