Saturday, 20 June 2015

Mbowe aonya tabia ya wanasiasa kuwagawa wananchi

Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe amewataka watendaji wa serikali kuacha tabia ya kuwagawa wananchi kwa itikadi za vyama vya siasa kwani kazi ya watendaji wa serikali ni kuleta maendeleo na kutekeleza ahadi za serikali siyo kuisaidia serikali katika siasa huku akitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu kesi yake iliyo malizika hivi karibuni.
Mhe Freeman Mbowe ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliyo fanyika katika viwanja vya stand ya zamani wilayani Hai  alipokuwa anakabidhi gari la kisasa la kukusanya na kusaga taka katika halmsahauri ya Hai na kisha kutoa angalizo ilo kwa watendaji wa serikali na kuwataka wakazi wa Hai wasiwe na wasiwasi juu ya hatima yake kisiasa.
Kwa upande wao wabunge wa viti maalum Chadema Rose Kamili kutoka mkoa wa Manyara amesema anashangaa kuona bado viongozi wa serikali wanatunga mbinu chafu za kuwakandamiza wapinzani bila sababu huku Cecilia Pareso kutoka Arusha akiwataka watendaji hao kutafuta mbinu za kuzuia ufisadi unao hibuka kila kukicha badala ya kuwaandama wapinzani wanao saidia jamii kujitambua.
Image result for mbowe na gari la taka 
Akiwatoa hofu wakazi wa Hai kuhusu hatima ya kisiasa kwa mbunge wao wakilii maarufu Jonathani Mdeme amesema hakuna kizuizi kwa Mhe Mbowe katika kuendelea na masuala ya kisiasa.

No comments: