Maafisa wa polisi waliwatia mbaroni washukiwa wawili wa ugaidi waliokuwa wakijaribu kuingia nchini Kenya kwa lengo la kuwachukuwa wanawake wanaotaka kujiunga na kundi la Al-Shabaab.
Waziri wa Ulinzi nchini Kenya Joseph Nkaissery, alitoa maelezo na kuarifu kwamba washukiwa hao wawili wa ugaidi waliowekwa chini ya ulinzi watafikishwa mahakamani wiki ijayo.
Akifahamisha kukamatwa kwa washukiwa hao katika mpaka wa Isebania ulioko kwenye kaunti ya Migori, Nkaissery alisema, ‘‘Washukiwa wawili walikamatwa wakati walipokuwa wakijaribu kuingia nchini Kenya kwa ili kuwafuata wanawake wanaotaka kujiunga na kundi la Al-Shabaab. Polisi walifanikiwa kuwakamata kwa ushirikiano wa raia pamoja na idara ya upelelezi.’’
Hapo awali, viongozi wa serikali ya Kenya waliwahi kutoa tahadhari ya uwezekano wa kutekelezwa kwa mashambulizi ya kigaidi na kundi la Al-Shabaab katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Tangu tahadhari hiyo kutolewa, serikali ya Kenya imechukuwa hatua thabiti za usalama dhidi ya ugaidi kote nchini.
No comments:
Post a Comment