Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi ameyasema hayo jijini
Dar es salaam wakati akizindua rasmi uuzwaji wa hisa za Asasi ya kifedha
ya YETU Microfinance P.L.C, ambapo alinunua hisa 40,000 zenye thamani
ya shilingi milioni 20, ili kudhuhirishia imani yake kwa asasi hiyo
iliyoasisiwa na Watanzania.
Dr Mengi pia amewahamasisha wajasiriamali kujitokeza kwa wingi
kununua hisa za asasi hiyo, na kuwataka wajibidishe katika kuusaka
ujajiri kwa njia zinazompendeza Mwenyezimungu.
Mapema Mkurugenzi wa Yetu Microfinance P.L.C Bw. Altemius Millinga
alisema asasi ya fedha ya Yetu Microfinance P.L.C imepata kibali
kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, cha kuuza hisa zipatazo
milioni 25 kwa shilingi 500 kila moja, katika kipindi cha kati ya Juni
18, 2015 na Julai 30, 2015. Kwa sababu hiyo amewahimiza wajasiriamali
kuchangamkia hisa hizo, ambapo kima cha chini cha ununuzi ni ni hisa
200 zenye thamani ya shilingi laki moja.
Wakati wa uzinduzi huo wajasiriamali wawili Bi. Johari Mkonde na
Bi Lucia Kimamba walitoa ushuhuda wa jinsi walivyofanikiwa katika
ujasiriamali wao.
No comments:
Post a Comment