Wednesday 17 June 2015

Kundi la Udugu wa Kiislamu lalaani hukumu dhidi ya Mursi

nullKundi la Udugu wa Kiislamu nchini Misri limesema hukumu za kifo dhidi ya rais wa zamani Muhammed Mursi na watu wengine kadhaa zilizotolewa leo hii na mahakama nchini humo ni batili.Kundi hilo limetowa wito kwenye mtandao wake wa Facebook kutaka wananchi washiriki katika maandamano ya umma hapo Ijumaa kupinga hukumu hizo, kushikiliwa kwa wat, kutekwa nyara na kutoweka kwa watu. Mahakama nchini Misri leo hii iliyakinisha hukumu ya kifo iliokuwa imetolewa dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa kwa kula njama za kukimbia gerezani na kushambulia polisi wakati wa vuguvugu la uasi la mwaka 2011 lililopelekea kuanguka kwa utawala wa Rais Husni Mubarak.Mahakama hiyo pia imemhukumu Mursi kifungo cha maisha gerezani kwa madai ya kuzifanyia upelelezi kundi la Kipalestina la Hamas, Hezbollah la Lebanon na Iran.

No comments: