Sunday, 14 June 2015

Waziri Bernard membe azuru kaburi la hayati Abeid Aman Karume

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati alipotembelea chumba ambacho muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume aliuawa kwa risasi wakati akicheza bao, katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho. Picha zote na John Badi
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mkonge (kulia), wakati alipotembelea chumba ambacho muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume aliuawa kwa risasi wakati akicheza bao, katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto) akishiriki katika dua ya kumuombea muasisi wa mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume, wakati alipotembelea kaburi lake lililopo katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati mbele) akifurahia jambo na makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waasisi wa mapinduzi ya Zanzibar, baada ya kutembelea kaburi la muasisi wa mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Aman Karume lililopo katika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui mjini Unguja Juni 13.2015 jioni, ambapo Waziri Membe yupo Zanzibar kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

No comments: