Sunday 14 June 2015

Lowasa aendelea kujikusanyia wadhamini Lukuki huko Rukwa

Waziri mkuu wa zamamni Mh Edward Lowasa ameendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Katavi na Rukwa na kupata   maefu wadhamini na amewataka waananchi waliojiandikisha kutunza vizuri shahada zao kwani ndio tiketi ya kuwawezesha kufikia ndoto zao za kuchagua kiongozi wanayemtaka.
Mh Lowasa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda na kupata mapokezi kishindo na wadhamini zaidi ya elfu tatu amewashukuru wote waliompokea na kuwataka kuendelea  kuhamasishana kujiandikisha na baadaye kupiga kura muda ukifika.
 
Awali mwenyekiri wa CCM wa mkoa wa Katavi Bw Mselem Saidi Abdllah amewataka wanaccm kote nchini kuwatendea haki wagombea wote wanaotafuta wadhamini kwani kwa vyovyote  vile mmoja wao ndiye atakayekuwa kiongozi wao.
 
Mh Lowasa ambaye pia ametembelea mkoa wa Rukwa na kuendelea kupata wadhamini wengi anaendelea kutafuta wadhamini katika mkoa wa Kagera.

No comments: