Zaidi
ya vijiji 14 wilaya ya kahama mkoani Shinyanga vinavyouzunguuka mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu vinakabiliwa na ukosefu wa huduma bora za afya
kwa muda mrefu na hivyo kusababisha wananchi kufuata huduma hiyo kwa
umbali wa zaidi ya kilometa 75 huku waathirika wakubwa wa hali hiyo ni
kinamama wajawazito na watoto.
Vijiji hivyo vya kata za Bugarama,Bulyanhulu na Mwingiro vyenye
zaidi ya wakazi 47,000, wananchi wamekuwa wakiwaomba bila mafanikio
viongozi mbalimbali kushughulikia tatizo hilo ambalo limekuwa ni tishio
kubwa kwa usalama wa afya zao.
Wakizungumza na ITV baadhi ya wananchi wa kata za Bugarama na
Bulyanhulu wamesema bado tatizo hilo la ukosefu wa huduma bora za afya
limekuwa likiwasumbua kwa kiasi kikubwa licha ya kuwepo kwa zahanati
moja ambayo haikidhi mahitaji hususani ya ongezeko la watu huku kinamama
wajawazito wakipata usumbufu mkubwa katika kutafuta huduma za upasuaji
zinapohitajika.
Aidha katika kusaidia kukabiliana na hali hiyo kampuni ya ACACIA
inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imeamua kujenga kituo kikubwa
cha afya kinachogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 kwa awamu ya
kwanza ikiwa ni moja ya muendelezo wa kusaidia huduma za kijamii kwa
vijiji vinavyouzunguuka mgodi huo wa dhahabu ambapo pia kampuni hiyo ya
acacia mbali ya kuchangia pato kubwa serikalini wastani wa dola za
kimarekani milioni 62 kwa mwaka lakin imekuwa ikishiriki vema miradi ya
ujirani mwema katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii katika
sekta za elimu,kilimo na maji.
No comments:
Post a Comment