Balozi wa Burundi katika umoja wa mataifa amekariri kuwa uchaguzi utaendelea mbele Jumatatu licha ya shinikizo uahirishwe
Balozi
wa Burundi kwenye umoja wa mataifa amesema kuwa uchaguzi utaendelea
jinsi ulivyopangwa siku ya jumatatu licha ya ombi kutaka uahirishwe
kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon.
Ban anasema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Burundi kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea huko. Balozi Albert Shingiro aliuambia mkutano wa
usalama wa umoja wa mataifa kuwa watu wanataka uchaguzi ufanyike.
Balozi Albert Shingiro aliuambia mkutano wa usalama wa umoja wa mataifa kuwa watu wanataka uchaguzi ufanyike.
Vyama vya upinzani na mashirika yasiyokuwa ya serikali tayari yametangaza kuwa watasusia uchaguzi huo.
Waandamanaji
wanapinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania urais kwa muhula
wa tatu wakidai kuwa inakiuka katiba ya Nvhi hiyo. Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa kufanyika Jumatatu
Rais Nkurunziza naye
anashikilia kuwa awamu ya kwanza aliteuliwa na wajumbe wala sio raia
kama vile inavyohitajika kwenye katiba iliyoundwa baada ya makubaliano
ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenye nchini humo.
Takriban
watu 50 wameuawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka huu wakati
rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu. Maandamano yalitibuka mjini Bujumbura baada ya
Pierre Nkurunziza kutangaza kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu
Maelfu ya raia wengine wa Burundi nao wamehamia mataifa jirani kwa hofu ya kuzuka mamchafuko zaidi.
Uchaguzi wa ubunge unatarajiwa siku ya Jumatatu huku uchaguzi wa urais ukipangiwa kufanyika tarehe 15 Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment