Wednesday 17 June 2015

Basi lililobaba wachezaji wa Taifa stars lapigwa Mawe

Watu wanaosadikiwa ni washabiki wa timu ya Taifa ya Tanzania wamelishambulia kwa mawe basi la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam 
Basi hilo lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakitoka mazoezini uwanja wa Karume, lilishambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wenye hasira waliochoshwa na matokeo ya timu hiyo ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Mholanzi, Martinus Ignatius "Mart" Nooij 
Toka kocha huyo wa Tanzania kutua nchini ameongoza Taifa stars mechi 17 ameshinda 4 na kufungwa mechi 13 matokeo ambayo hayajawaridhisha watanzania na wapenda soka kwa ujumla
Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.
Alizungumzana mandishi wetu kwa Njia ya simu Rais wa TFF Malinzi amesema anawaomba watanzania wasiwakatishe nia wachezaji wawape mda kwani bado wanamchi mbeleni dhidi ya Uganda
Aliongeza kwa lusema Kuwa endapo Taifa stars itashindwa kuibuka na Ushindi dhidi ya Uganda basi Kocha wa kikosi hicho Mart Nooij afungashie virago akiwa huko huko Uganda kwani TFF haita kuwa tayari kuona Tanzania ikifungwa tena 

No comments: