Umoja
wa Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika
uchaguzi wa wabunge wa Burundi utakaofanyika Jumatatu kwa sababu
masharti ya uchaguzi huru na wa haki hayajazingatiwa.
Vyama vya
upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza
wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.Mapema Jumapili, Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma alisema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.
No comments:
Post a Comment