Aliyekuwa kocha wa Simba Goran Kopunovic akitoa maelekezo kwa kiungo wa klabu hiyo Said Ndemla |
Klabu ya soka ya ‘Wekundu wa
Msimbazi’ Simba imeendelea kulipiga danadana suala la kumtangaza kocha
mpya atakaechukua nafai ya Goran Kopunovic ambapo uongozi wa timu hiyo
umesema unatarajia kumtangaza mapema mwanzoni mwa juma lijalo.
Afisa habari wa klabu hiyo Hajji
Manara amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuendelea kuwa
wavumilivu huhu akisema, tayari wameshampat kocha kilichobaki ni
kumtangaza tu.
“Kocha tutamtangaza wiki ijayo,
kwasababu tumeshampata, sisi wiki ijayo tutamtangaza rasmi. Jumamosi
mimi natoa ‘press release’ nikishatoa tutawaeleza tutamtangaza lini,
lakini Jumamosi natoa press release”, amesema Manara.
“Ishu ya kwamba tumemtoa nchi
gani inakuwa siyo ‘story’ tena itakuwa imeshapwaya hiyo. Watu wawe na
subra Jumatatu siyo mbali”, ameongeza Manara.
Juma lililopita Manara alisema,
wamepanga kumtangaza kocha mpya wiki hii lakini Manara ametoa taarifa
nyingine akisema kocha huyo atatambulishwa wiki ijayo. Siku chache
zilizopita, mwenyekiti wa usajili wa klabu hiyo Zacharia Hans Poppe
alisema, kocha waliyempata kurithi mikoba ya Kopunovic ni raia wa
Uingereza.
No comments:
Post a Comment