Saturday 20 June 2015

Dk. Bilali "sekta binafsi ina nafasi ya kuwezesha Tanzania kupiga hatua katika sekta ya ujenzi."

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr.Mohamed Gharib Bilal amesema sekta binafsi ina nafasi kubwa ya kuiwezesha Tanzania kupiga hatua katika sekta ya ujenzi na kuwa miongoni mwa nchi zenye makazi bora kwa wananchi wake endpo itashirikishwa na kuungwa mkono ipasavyo.
Makamu wa rais Dr.mohamed Gharib Bilali ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mradi wa nyumba uliotekelezwa na AVIC COAST LAND DEVELOPMENT TANZANIA LIMITED na kuongez kuwa seikali inaunga mkono mpango wa ujenzi wa makazi bora kwa watanzania kwa kuwa mpango kama huo unaleta mvuto mpya kwa kizazi kipya ambapo Tanzania ya leo na ya kesho itajivunia kwa kuwa namakazi bora.
Kwa upande wake balozi wa china hapa nchini amesema miradi ya ujenzi wa makazi bora itasaidia kuongeza idadi ya ajira kwa vijana wakitanzania ambapo ndani ya miaka mitano kunatarajiwa kuwa na idadi kubwa ya ajira kupitia miradi kama hiyo na hivyo kusaidia serikali ya Tanzania kupambana na tatizo la ajira nchini.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa AVIC hapa nchini amesema makazi mazuri yana saidia umarisha maisha na hivyo kuwa na kizazi ambacho kinafurahia maisha kwa kuuwa na makazi bora lakini pia afya bora.

No comments: