Gavana wa zamani wa jimbo la Florida, Jeb Bush, mtoto na kaka wa
marais wa zamani wa Marekani, ametangaza rasmi kuingia katika mbio za
urais.
Bwana Bush, ametangaza nia yake jana Jumatatu, na kuwa mgombea wa 11 katika chama cha Republikan, huku ikitazamiwa wagombea wengi zaidi kujitokeza.
Wakati anatangaza nia yake hiyo, alishangiliwa na wafuasi wake mjini Miami, Florida, na kudai Marekani ipo katika muelekeo mbaya.
Amelaumu chama cha Demokrat, kwa kuifanya nchi kuwa ni ya kusimamiana, na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi.
Amesema kwamba Marekani inahitaji rais atakayekuwa tayari kusitisha utamaduni uliopo sasa Washington, na yeye ndiye anayestahili kuongoza.

No comments:
Post a Comment